Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Msumbiji ameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Afrika, akiungana na Mabalozi wa nchi nyingine za Afrika waliopo Jijini Maputo kuanzia tarehe 22 hadi 25 Mei, 2024.

Maadhimisho hayo yamefanyika chini ya Kaulimbiu “Elimisha Mwafrika anayefaa katika Karne ya 21″ ambapo Mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi rasmi tarehe 22 Mei, 2024 alikuwa Mhe. Carmelita Rita Namashulua, Waziri wa Elimu na Maendeleo ya Watu wa Jamhuri ya Msumbiji.

Aidha, katika Maadhimisho hayo Mabalozi wamepata nafasi ya kutembelea Chuo cha Mafunzo ya Walimu Chibututuine kilichopo Wilaya ya Manhica na kujionea jitihada zinazofanywa na Serikali ya Msumbiji kuwaandaa walimu wa Shule za Msingi.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa tarehe 25 Mei, 2024 kwa matukio mbalimbali ikiwemo mechi ya mpira wa miguu baina ya Mabalozi wa Afrika na Viongozi wa Serikali ya Msumbiji. Mhe. Balozi Kasike pia alishiriki kwenye mechi hiyo ambapo Mabalozi wa Afrika walishinda kwa mabao 3 – 2.

By Jamhuri