Wizara ya Ujenzi katika mwaka wa fedha 2024/25, imetenga kiasi cha Sh bilioni 9.7 kwa ajili ya mradi wa kupunguza msongamano barabara za Dar es Salaam.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema fedha hizo ni kwa ajili ya mradi huo .

“Mradi huu umetengewa jumla ya Sh milioni 9,781.49 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa barabara ya Goba – Matosa – Temboni (km 6), kuanza ujenzi wa barabara za Kibamba – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (Km 14.66), Kongowe – Mjimwema – Kivukoni Ferry (One Lane Widening: km 25.1);

“Kuanza upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki (km 16.4) pamoja na kuanza ujenzi wa barabara za Mji Mwema – Kimbiji – Pembamnazi (km 10), Kipata (m 700), Livingstone (m 170), Msikitini – Sharif Shamba (m 540), Kibamba Shule – Mpiji Magoe (km 9.2), Mbezi Victoria – Mpiji Magoe – Bunju (km 11), Chanika – Mbande (km 3), Mbezi Msakuzi – Makabe Jct (km 7) na Kimara – Bonyokwa – Kinyerezi (km 7),” amesema na kuongeza:

“Fedha hizi pia zitatumika kulipa madeni ya makandarasi wa barabara za Mbezi – Malambamawili – Kinyerezi – Banana (km 14), Mbezi Mwisho – Goba (km 7), Tangi Bovu – Goba (km 9), Kimara Baruti – Msewe – Changanyikeni (km 2.6), Banana – Kitunda – Kivule – Msongola (km 14.7): sehemu ya Kitunda – Kivule (km 3.2).

“Ardhi – Makongo – Goba: sehemu ya Goba – Makongo (km 4), Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi/Morogoro Road (Mbezi Mwisho); sehemu za Madale – Goba (km 5) na Wazo Hill – Madale (km 6) pamoja na Ardhi – Makongo – Goba; sehemu ya Ardhi – Makongo (km 5),” amesema.