Barrick, Polisi washiriki matembezi ya kupinga vitendo vya ukatili Dar

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za wilaya ya Kinondoni na wananchi wakishiriki matembezi ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ikiwa ni maadhimisho ya siku  16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika matembezi ya kupinga  vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Barrick kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na Maofisa kutoka Jeshi la Polisi.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania,Georgia Mutagahywa,akiongea na washiriki  wa maandamano yakupinga vitendo vya ukatili yaliyofanyika jana jijini  yaliondaliwa na kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi dawati la jinsia.Wengine pichani ni Maofisa kutoka Jeshi la Polisi na Serikali
Katibu  Tawala  wa Wilaya ya Kinondoni  Stella Msofe (kushoto) akiongea wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto yaliyoandaliwa na Kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na  Dawati la jinsia la Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni  jijini Dar es Salaaam yaliyofanyika jana katika viwanga vya kituo cha Polisi cha Oysterbay. Katikati ni Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa na  Kamishna Msaidizi wa Polisi( ACP)  Alyoce  Nyantora ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP,  Camilius Wambura