Joyce NdalichakoKaulimbiu ya nchi inayozipaisha nchi zilizoendelea kiuchumi ni: Sayansi, teknolojia, ugunduzi, ubunifu na demokrasia. Nasi, sharti hii iwe ndiyo kaulimbiu yetu na siyo demokrasia peke yake.

Ni vyema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia (Ubunifu) na Ufundi kwa kushirikiana  mashirika ya hifadhi ya jamii kama NSSF, PSPF, LART na mashirima mengine kama NHC, UTT, GEPF n.k. na michango ya wananchi,  kwa kutumia mboni ya ziada yanaweza kufanikisha hili na mengine nitakayoyaeleza kwa ufupi. Hivyo Wizara ya Elimu iende mbali kwa kufanya lifuatalo:

 

 Kujenga chuo Kikuu cha Ubunifu cha Tanzania (NASA ya Tanzania)

1.1 Kwa kushirikiana na wadau wa ubunifu hasa COSTECH, Wizara ijenge Chuo Kikuu cha Ubunifu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuboresha bidhaa za wabunifu na utafiti mbalimbali na kutengenezwa kuwa bidhaa za kuuzwa ndani na nje ya nchi katika nyanja zifuatazo:  Mitambo (magari, ndege, treni, meli);   mitambo ya kuboresha: Chakula, vinywaji, dawa na vifaa vya hospitali, madini, mafuta, gesi, mifugo, wanyamapori na misitu; mitambo ya umeme, elekroniki n.k. 

Kwa mtazamo wangu, chuo kikuu  hiki inafaa NSSF iingine ubia na TATC (Nyumbu) na kijengwe katika eneo la Nyumbu maana ni eneo kubwa na kwa kuwa TATC inamilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Chuo Kikuu cha Ubunifu, kitakuwa chini ya uangalizi na nidhamu ya Jeshi letu.

1.2 Viwanda vichache nchini vinatumia mitambo ya kizamani sana kiasi kwamba mitambo yake haiwezi kushindana na viwanda vya nchi zilizoendelea katika kuzalisha bidhaa shindani.

Lakini hata kwenye ulinzi na usalama, kwa sababu unanunua silaha, unakuwa kiulinzi hauna siri maana yule aliyekuuzia anaweza kutoa siri ya silaha zako kwa adui yako kutegemeana na masilahi yake (muuzaji).

Tuchukue mfano wa Kampuni ya Katani Ltd iliyopo Tanga. Binafsi nilitembelea kiwanda chake tanzu cha kutengeneza bidhaa zinazotokana na mkonge. Ni bidhaa nzuri sana. Lakini mitambo yake ni ya zamani mno. Kama ingekuwa na mitambo ya kisasa, ingetoa bidhaa shindani duniani.

Tanzania ingekeuwa na viwanda vya kisasa vya kutengeneza mitambo ya kuchakata mkonge, kwa hakika kiwanda kingekuwa mbali sana. Aidha, nilizuru ubunifu wa Katani Ltd kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia katani-taka. Kwa kukosekana mfumo wa ubunifu nchini mwetu, hadi sasa Tanzania tumeshindwa kuufanyia kazi na kuutumia ubunifu huu muhimu japo tuna malighafi (katani-taka) nyingi mno.

Ndiyo maana wakati wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere pamoja na kujenga taasisi mbalimbali za utafiti, alijenga kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Ltd ili kiwe kinazalisha mitambo ya kutumika katika ujenzi wa wiwanda vipya nchini mwetu (na kuuza nchi za nje). Kwa maneno mengine, kiwe kiwanda cha kuzalisha viwanda vingine.

Na ieleweke, nchi ambayo inategemea wakati wote kununua mitambo ya viwanda vyake haiwezi kuendelelea kwa sababu zilizo wazi. Ni dhahiri katika kuanza tutaanza na mitambo ya kununua, lakini tukiwa na mikakati hai na bunifu ya kutengeneza mitambo yetu wenyewe, hapo tutafika tulikkusudia kufika.

 1.3 Tanzania ina taasisi za ubunifu na watu wabunifu ambao wamebuni bidhaa mbalimbali, lakini hadi sasa ubunifu huo upo upo tu. Taasisi za ubunifu zimefanya utafiti mbalimbali ambao una manufaa kwa taifa letu. Lakini utafiti huo unaozea katika mafaili. Kujenga chuo cha ubunifu ndiyo mwarobaini wa kufanya ubunifu na utafiti huu ukue na kufikia uzalishaji mkubwa viwandani.

1.4  Wizara ya Elimu ishirikiane na Wizara ya Viwanda kupotia Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) katika kila mkoa,  vigeuzwe  kuwa vituo vya mikoa vya ubunifu kama vitengo vya Chuo Kikuu cha Ubunifu badala hali ya sasa ambako ni karakana  za vifaa  vya kawaida mno.

1.4 Chuo kikii cha Ubunifu, kitaongeza “Multiplier effect” katika nyanja ya kiuchumi na kijamii kuliko jumla ya miradi yote iliyopo nchini kwa sababu itakuwa ni kiini cha ujenzi wa viwanda imara nchini na kuuza mitambo ya viwanda nje ya nchi.

Kutokana na maelezao yaliyopo hapo juu, napendekeza katika suala hili kuongeza matamko yafuatayo:

 

3.2.9 Serikali itahakikisha bidhaa zote zinazotokana na wabunifu na utafiti mbalimbali zinaboreshwa na kutengenezwa kibiashara na kuuzwa nchini na za nchi nje.

 3.2.10 Wananchi wote ambao utafiti, ubunifu au mawazo yao yatalinufaisha taifa kiuchumi au kijamii baada ya kuboreshwa na kuwa bidhaa, au vyovyote vile, watapewa tuzo itakayokuwa na fedha na kupewa mrahaba wakati wote ambao utafiti, ubunifu au wazo lao litaendelea kulinufaisha taifa.

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema:

Athari za ujinga, umasikini na ugonjwa

Ujinga, umasikini na ugonjwa ni chanda na pete na huishi pamoja.

· Hivyo, kwa kupambana na umasikini, huongeza uzalishaji wa mali wakati huo huo unakuwa na jamii yenye afya bora.

· Ukiwa na jamii iliyoelimka, unaongeza uwazi na hivyo kudumisha amani na utulivu.

· Kama tuna dhamira ya dhati jamii ya Mkoa wa Kigoma na Tanzania nzima iwe na hali nzuri kiuchumi, kijamii na kiafya tunachotakiwa kufanya ni kupambana ili kuondoa umasikini kwa kuwapa wanajamii elimu bora.

Ni elimu pekee inayoweza kuleta uwazi, hivyo elimu ni ufunguo wa: Afya nzuri, amani na utulivu na kwa sababu hiyo, elimu inatakiwa uwepo utaratibu  rafiki wa kupatikana kwa wote kwa kiwango na ubora  ulio sawa.

 

Hitimisho

 Kwa vile mapendekezo haya yatawagusa Watanzania wote, Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia (Ubunifu) na Ufundi iandae mdahalo wa kitaifa  kupata maoni mapana ya  wadau  ili utekelezaji wake uwe wa ufanisi wa hali ya juu kwa manufaa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa taifa letu la Tanzania.

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema: “Waliofanikiwa hawakufanya mambo tofauti, bali waliyafanya tofauti.”

MUNGU AWABARIKI

 

 Mwandishi wa makala hii, Leonard Ndimubansi, ni msomaji mahiri wa JAMHURI. Anapatikana kupitia simu: 0713363351/0766687356; e-mail: [email protected]

By Jamhuri