Jumla ya tani 2,284 za ufuta ghafi kutoka kwa wakulima wa halmashauri za Mtama, Lindi na Kilwa Mkoani Lindi wanaohudumiwa na chama kikuu cha ushirika Lindi Mwambao zimeuzwa katika mnada wa kwanza uliofanywa na chama hicho kwa bei ya juu ya shilingi 4,021 na bei ya chini shilingi 4,005.

Mnada huo umefanyika Juni 10, 2023 katika chama cha msingi cha ushirika Milola ambapo jumla ya wanunuzi 21 wamejitokeza kuomba kununua ufuta huo.

Awali akizindua mnada huo wa kwanza, mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewasisitiza wakulima kutumia fedha watakayoipata katika kuboresha maisha yao huku mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Lindi Secilia Sostenes akiwahimiza wanunuzi kuwalipa wakulima mapema sambamba na kutoa mzigo wao mapema kwenye maghala.