Na Mathias Canal, Bukombe-Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kutoa fesha kiasi cha shilingi 300,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya Wilaya ya Bukombe.

Mradi huo unatarajiwa kutoa huduma za dharura kwa jamii na wasafiri wanao tumia barabara kuu inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi huku kiasi cha wananchi wapatao 100,051 watahudumiwa.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko ameyasema hayo leo tarehe 6 Agosti 2023 mjini Bukombe wakati akizungumza na wananchi mara baada ya mwenge wa uhuru kuzindua jengo la ICU Wilaya ya Bukombe.

“Nafurahi kusema kwamba serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha watu mahututi (ICU) ili tuache kuwapeleka watu wetu mbali kwa ajili ya huduma hiyo badala yake waipate hapa hapa” Amekaririwa Dkt Biteko na kuomgeza kuwa

“Ndugu kiongozi wa mbio za mwenge Tufikishie salamu zetu kwa Rais, mwambie mama kwenye kazi uliyoifanya Bukombe katika kila sekta watu wale wamekuandalia maua yako”

Mhe Biteko amesema kuwa Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi huku akimshukuru pia kwa kutenga fedha kwa ajili ya Ujenzi wa chuo cha VETA Bukombe.

By Jamhuri