Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko, akizungumza  wakati  akiwasha umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai,akizungumza wakati wa tukio la kuwasha kwa  umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa tukio la kuwasha kwa  umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo,Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Naibu  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko,(hayupo pichani) akizungumza kabla ya kuwasha  umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko,akizungumza  wakati  akiwasha umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

……………………………………………………………..

Na James Nestory, JamhuriMedia, Kongwa

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko amesema adhma ya serikali ya Awamu ya Sita ni kufikisha umeme katika kila kitongoji kabla ya uchaguzi wa 2025.

Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati  akiwasha umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

Dkt. Biteko amesema kuwa Rais Dkt. Samia anapambana usiku na mchana kuhakikisha umeme unapatikana na kuinua hali za maisha ya wananchi waliopo vijijini kwani umeme sio anasa bali ni jambo la muhimu kwa sasa.

“Katika sekta ya umeme tutafanya kila kupeleka umeme katika kila kitongoji kupeleka umeme katika kila eneo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 katika uongozi huu wa serikali ya Awamu ya Sita umeme sio anasa bali ni jambo la lazima.”amesema Dkt.Biteko

Aidha, amewaagiza TANESCO na REA kuhakikisha Vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na umeme kuhakikisha vinawekewa huduma hiyo muhimu kwa haraka

Katika hatua nyingine Biteko amesema serikali inaendelea na mikakati ya kuboresha nishati ya kupikia kwa kuboresha gharama za gesi na majiko ya kupikia

Kwa upande wake Mwakikishi wa Meneja wa Wakala wa Nishati Vijiji (REA), Mhandisi Thomas Mbaga amesema Mkoa wa Dodoma Una jumla ya vijiji 580 ambapo vijiji 410 sawa na asilimia 70 vimepatiwa huduma ya umeme kupitia miradi ya REA.

Amesema REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Dodoma lengo ni kuwafikishia huduma bora wananchi ili kuboresha huduma za jamii.

“Kwasasa REA inaendelea na mikakati wa kupeleka umeme katika migodi midogo na maeneo ya kilimo ambayo hayajafikiwa na umeme ambapo katika hatua hii migodi 13 itafikiwa katika wilaya za Mpwapw, Chamwino,Bahi, Dodoma na Kondoa.

Ameongeza kuwa :”REA itaendelea kuwasimamia Kwa ukaribu wakandarasi wanaotemeleza miradi ya umeme ili kukamilisha kwa wakati na Kwa ubora unatakiwa ili iliweze kuwanufaisha wananchi kama ilivyopangwa,”.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ameishukuru TANESCO na REA kwa kazi kubwa inayofanywa katika mkoa huo ya kuhakikisha umeme unapatikana pamoja na usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya wilaya hiyo zinazotolewa na Mhe. Rais Samia.

 ”Mahitaji ya umeme kwa Mkoa wa Dodoma ni makubwa na kumekuwa na ongezeko la viwanda na shughuli za kiuchumi hivyo ni vema taasisi hizi zikafanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo kwa wanachi.”amesema Mhe.Senyamule

Awali Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Mhe. Job Ndugai ameikumbusha REA kupeleka umeme kwa wakati katika maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa na nishati hiyo hususan vitongoji vya Chinangali, Chamwino na Manzese na kuwataka TANESCO na REA kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma hiyo ya umeme.

“Tunashukuru sana jitihada za Mhe. Rais Samia kutenga fedha kwa ajili ya masuala ya nishati, hii imekuwa na msaada mkubwa kwa wananchi wa Kongwa hususan katika kuleta maendeleo ya wananchi wetu,” amesema Mhe. Ndugai.

Mradi huo wa maji uliasisiwa na Mwalimu Abdi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Mtanana na tayari visima 25 vimeshawekewa umeme ili wananchi wapate huduma bora katika wilaya hiyo.