Chama Cha Wananchi (CUF) kimeendelea kupata pigo, baada ya madiwani wake wawili kujivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Madiwani hao wa Kata ya Kilindoni, Hamad Musa na Hassani Mohammed wa Kata ya Jibondo wilayani Mafia wamesema wamefanya uamuzi huo baada ya kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Please follow and like us:
Pin Share