August 19,2018 Rais Magufuli amepata msiba kwa kufiwa Dada wa yake Marehemu Monica Magufuli amabye amefariki akiwa na umri wa miaka 63, ameacha watoto 9, pamoja na Wajukuu 25. Viongozi mbalimbali wametoa pole kwa Rais Magufuli kupitia mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kupitia ukurasa ameandika “Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na wana CHADEMA wote, natoa pole na salaam za rambi rambi kwa Rais Magufuli kwa kufiwa na dada yake Monica Magufuli. Mungu awape faraja, na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.”

Nae aliyekuwa Mbunge wa CCM na Waziri wa zamani wa Maliasili Lazaro Nyalandu ameandika hivi “Natoa pole kwa Rais Magufuli na familia yake kwa kufiwa na dada yake mpendwa, Monica Magufuli. Hakika, maisha yana thamani kubwa. MUNGU awafariji, na ampe dada yetu pumziko la milele mahali pema peponi, AMINA.”

Please follow and like us:
Pin Share