Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amefariki dunia hii leo, Februari 10, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar es Salaam..

Taarifa ya kifo chake imetangazwa leo na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Lowassa alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 2005 hadi 2008 chini ya uongozi wa Dkt. Jakaya Kikwete.

Edward Ngoyayi Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 ambapo aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha kwa tikeyi ya Chama Cha Mapinduzi ambapk a.

Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa 10 tarehe 30 Desemba 2005 na akajiuzulu Februari 7, 2008 kwa kashifa ya Richmond.

Mwaka 2015 alikuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

By Jamhuri