Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga umeungana na Serikali na wadau wengine kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo umeandaa kampeni ya kutoa elimu dhidi ya vitendo hivyo katika shule za msingi na sekondari zilizopo katika vitongoji vilivyopo jirani na mgodi huo.

Kupitia kampeni hiyo wanafunzi walipata fursa ya kufundisha jinsi ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia sambamba na kuuliza maswali kutoka kwa wataalamu wa ustawi wa jamii na jinsia waliokuwa wakiendesha maswali hayo,pia waligawiwa vipeperushi na t-shirt zenye jumbe za kukabiliana na vitendo hivi ambavyo vimekithiri katika jamii.

Akiongea kwa niaba ya Wananchi kuhusu maadhimisho haya Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyanhulu, Abdallah kombo,alishukuru Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha kampeni hizi ambazo kwa kiasi kikubwa zimeweza kuwajengea uwezo wanafunzi kuelewa jinsi ya kujikinga na vitendo hivyo.

…………………………………………………………………..

Wanafunzi wa shule za sekondari Bugalama na Bulyanhulu wakifuatilia mafunzo ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Mgodi wa Bulyanhulu


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bulyanhulu iliyopo wilayani Msalala wakifurahia vipeperushi na T shirt walizogawiwa wakati wa  kampeni ya uhamasishaji wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia iliyoendeshwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu shuleni hapo jana.  
Bi. Anna Boniphase mwakalinga Afisa Maendeleo ya Jamii kata Bulyanhulu akiongea na wanafunzi jinsi ya kujikinga na ukatili wa kijinsia

By Jamhuri