Na Isri Mohamed

Kiungo wa Brazil anayekipiga klabu ya Singida Fountain Gate, Bruno Barroso amethibitisha kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili kuanzia leo Machi 4, 2024.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bruno amepost barua yenye ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa Singida bila kutaja sababu hasa Iliyomfanya aombe kuvunja mkataba au wapi anapoelekea.

Bruno ameitumikia Singida kwa misimu miwili mfululizo, akiisaidia klabu kumaliza ikiwa ndani ya tano bora msimu uliopita.

Bruno atakumbukwa sana kwa utaalamu wake wa kupiga mipira iliyokufa, akiwafunga makipa bora akiwemo Aishi Manula wa Simba.

Bruno amewahi kuhusishwa na vilabu mbalimbali ikiwemo Yanga.

By Jamhuri