Garden Michael aanza kuwasha moto Afrika Kusini

Isri Mohamed

Mlinzi wa kushoto raia wa Tanzania, Gadiel Michael anayekipiga kwenye klabu ya Cape Town nchini Afrika Kusini ameanza kuwasha moto kwenye klabu yake hiyo kwa kutoa Assist ya bao la kwanza wakicheza dhidi ya Galaxy fc.

Mchezo huo ulimalizika kwa Cape Town kuvuna alama tatu kwa ushindi wa mabao mawili yaliyofungwa na Cupido na Maphathe.

Kufuatia ushindi huo klabu ya Cape Town inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini imeingia kwenye rekodi Kwa mara ya kwanza msimu huu ya kupata ushindi back to back na kufikisha alama 10 wakiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo, jambo linaloonesha mwanga na matumaini ya kusalia kwenye ligi.

Gardiel amesajiliwa Cape Town Stars kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Singida United.