Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Bondia Seleman Kidunda anatarajia kushuka dimbani leo usiku kupigana na Assemahle Wellem kutoka Afrika kusini.

Baada ya kupima uzito Kidunda ametoa ahadi kwa watanzania ya kulipa kisasi kwa Wellem ambaye miezi michache iliyopita alipata ushindi katika ardhi ya Tanzania mkoani Mwanza akimchakaza Twaha Kiduku.

“Namuheshimu bondia yeyote wa Tanzania na nje,Wellem ni bondia mzuri ila mimi ni mzuri zaidi yake, Nitamnyoosha, Naitwa Jiki dawa ya madoa watu waje kuangalia dawa ya madoa inafanya kazi gani” amesema Kidunda.

Mabondia wengine watakaopigana katika pambano hilo litakalochezwa usiku wa leo katika ukumbi wa Ware House Masaki, ni pamoja na mtanzania Nassib Ramadhan vs Lulu Kayage vs Jesca Mfinanga na wengine wengi.

By Jamhuri