Na isri Mohamed, JamhuriMedia

Klabu ya Yanga imefuzu na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwafunga CR Belouizdad mabao manne kwa Nunge.

Mabao hayo manne yamefungwa na Mudathir Yahya, Kennedy Musonda, Aziz Ki na Joseph Guede.

Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kutinga hatua hiyo baada ya miaka mingi.

Yanga wamefuzu kwenye kundi D wakiwa na slama nane wakitanguliwa na Al Ahly wenye alama tisa.