Category: MCHANGANYIKO
Wanariadha Kenya kuchunguzwa
Kenya imekosolewa na Shirika la Kudhibiti matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli kwa kukosa kufanya uchunguzi katika ongezeko la visa vya wakimbiaji wa Kenya wanaoshukiwa kutumia dawa hizo.
Malinzi: Simba kuweni na amani
Wiki iliyopita Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimpata rais mpya, Jamal Malinzi, anayechukua mikoba ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo, Leodegar Tenga, aliyeongoza kwa kipindi cha miaka ninane mfululizo.
Wakimbia makazi kukwepa operesheni okoa
Siku chache baada ya maofisa wanaoendesha Operesheni Okoa Mazingira iliyofanyika katika Kijiji cha Usinge wilayani Kaliua, kutuhumiwa kumuua, Kipara Issa (39), kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume na sheria, baadhi ya wanaume katika kijiji hicho wamelazimika kuzikimbia familia zao kwa hofu ya kukamatwa na maofisa hao.
Yah: Utitiri wa vyombo vya habari na habari inayotolewa
Kuna wakati nakumbuka miaka yetu ya giza totoro la habari, kwamba habari ilikuwa ni kitu nyeti ambacho mwananchi alipaswa kujua kwa gharama ya muda au kwenda safari kuitafuta, leo habari unaipata mahala ulipo na unachagua unataka habari gani.
Michael Jackson anaongoza kwa utajiri
Mfalme wa muziki wa aina ya Pop, Marehemu Michael Jackson, ametajwa kuwa kati watu maarufu duniani waliofariki dunia ambao kazi zao zimeingiza kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia Oktoba 2012 hadi Oktoba 2013.
Hammer Q auponda muziki wa Bongo Fleva
Mwimbaji Nyota wa Muziki wa Taarab nchini, Hussein Mohammed ‘Hammer Q’ (pichani kushoto) amesema kuwa alifanya muziki wa bongo fleva kama njia ya kutafuta njia ya kufanikiwa katika tasnia ya muziki.