TAKUKURU yawachunguza TBL

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeanza kufanya uchunguzi wa kina kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuthibitisha habari za kiuchunguzi zilizofanywa na gazeti hili la JAMHURI na kubaini kuwa TBL wanatumia udhaifu wa sheria kukwepa kodi nchini. Uchunguzi huo ulioanza kuchapishwa Machi 1, mwaka huu, unaonesha kuwa TBL wanakwepa kodi kwa njia…

Read More

Benki ya Ushirika K’Njaro matatani

Benki ya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KCBL) inakusudiwa kushitakiwa mahakamani kujibu tuhuma za kumdanganya mwanachama wa Benki ya Kijamii Vijijini (VICOBA) kuwa benki hiyo ingempatia mkopo wa Sh milioni 50. Mwanachama huyo, Vicent Mulamba, ameipa KCBL hati ya kusudio la kuifikisha mahakamani kwa kile anachodai ilimdanganya mkopo licha ya kutimiza masharti. Nakala ya barua hiyo…

Read More

Huawei wanasa mtego wa Serikali

Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana imeanza kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kubaini wafanyakazi raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini bila vibali. Wiki iliyopita, viongozi wa wizara hiyo walivamia ofisi za kampuni ya mawasiliano ya Huawei zilizopo eneo la Victoria na Makumbusho jijini Dar es Salaam, na kubaini wafanyakazi raia wa…

Read More

Chuo cha Mandela hekaheka

Ujanja ujanja kwenye mfumo wa mishahara ya watumishi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ya jijini Arusha, unatajwa kuwa chanzo cha Serikali kupoteza fedha nyingi. Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa mfumo wa ‘Lawson’ unaotumika kuandaa mishahara, umeingizwa taarifa potofu zinazosababisha upotevu wa fedha na watumishi kadhaa kupandishwa ngazi tatu za…

Read More

Dalali, TBA mikononi mwa Waziri Mkuu

Waliouza nyumba ya Serikali namba 162, kiwanja namba 1103 iliyoko Kitalu ‘S’ eneo la Mafiati jijini Mbeya kwa gharama ya Sh milioni 250 kwa mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, Saul Henry Amon, wamelalamikiwa kwa Waziri Mkuu. Nyumba hiyo ambayo kwa sasa ina hatimiliki mbili, moja ikiwa imetolewa kwa mtumishi wa umma aliyeuziwa nyumba na…

Read More

Polisi Oysterbay ilivyouzwa

Mkataba wa utwaaji wa eneo la Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam uliofanywa na kampuni ya Mara Capital kutoka nchini Uganda, unatajwa kuwa miongoni mwa mikataba hatari iliyotekelezwa wakati wa uongozi wa Awamu ya Nne. Mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma, akifungua kikao kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa Serikali…

Read More