Home Kitaifa Mbunge wa Chadema Azungumzia Hali ya Kisiasa kwa Upande Wake

Mbunge wa Chadema Azungumzia Hali ya Kisiasa kwa Upande Wake

by Jamhuri

Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Said Kubenea amewataka wananchi wa jimbo lake na nchi nzima kwa ujumla kupuuzia taarifa zinazosambazwa dhidi yake kuhusu yeye kutaka kukihama chama chake.

Kebenea amesema kuwa ataendelea kuwa Mbunge wa jimbo la Ubungo na hana mpango wowote wa kuondoka CHADEMA kuhamia CCM.

Kubenea ameyasema hayo baada ya kuibuka uvumi uliosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa mbunge huyo anataka kuhamia CCM.

Hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu kubwa la kisiasa ambapo wabunge pamoja na wanachama wa vyama mbalimbali wenye nyadhifa tofauti tofauti wakitangaza kujivua uanacham na kujiunga na chama kingine huku Chama Cha Mapinduzi CCM kikishuhudiwa kupata wafuasi wengi wanaokihamia.

You may also like