Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (CHADEMA) amekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara ndani ya CHADEMA
Kupitia mitandao ya kijamii imesambazwa barua inayodaiwa ni ya Mnyika ambayo imedai amejiuzulu nafasi yake ili aweze kupata muda wa kutosha kuwatumikia wapiga kura wake.

Mnyika masema barua hiyo ni batili na kuwataka wanachama wa CHADEMA na wananchi kwa ujumla kuipuuza kwani ina lengo la kupotosha umma na kuisambaratisha CHADEMA ambalo ni jambo litakuwa gumu sana kukisambaratisha Chama chetu, kwani chama chetu ni kikubwa sio kama wanavyofikiri.

By Jamhuri