JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Michezo

Wageni wanakuja, wanaondoka, makocha wa kwetu wapo tu

Achana na majina ya Sven van der Broeck wa Simba na Luc Eymael wa Yanga, tubaki na majina ya makocha wa hapahapa Afrika ili tuzungumze kitu kinachoeleweka. Hawa utawauliza tu nini kifanyike. Maana ukizungumzia kocha kutoka Malawi, Zambia, Kenya, Uganda,…

Kuna kazi ngumu

Serikali ya Hispania imefanya mabadiliko ya sheria ya haki za matangazo ya uonyeshaji wa mechi za soka kupitia vituo vya runinga. Ilipofika mwaka 2016, timu zote za Hispania zilikuwa na haki sawa kwenye suala la malipo ya haki za mechi…

Timu ikishinda ya wote, ikifungwa ya kocha

Mashabiki wa Liverpool wanaita ‘The Miracle of Istanbul” (muujiza wa Istanbul). Ni miaka 20 ilikuwa imepita tangu timu hiyo ilipotwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwaka 1985. Mhispania Rafael Benitez anawapa kombe hilo katika fainali dhidi ya AC Milan mwaka…

Simba, Yanga fupa lisilo na maana

‘Uzalendo umetushinda, uzalendo umetushinda’, hayo yalikuwa ni maneno yaliyosikika yakiimbwa na mashabiki wa Yanga mwaka 1993 baada ya Simba kufungwa na Stella Abidjan katika mechi ya fainali ya Kombe la CAF (sasa Kombe la Shirikisho). Stella Abidjan walishinda magoli 2-0…

Tunapomsifia Samatta, tumzomee Kichuya

Miaka 44 iliyopita Watanzania wengi tukiwa hatujui chochote kuhusu teknolojia wala televisheni, Sunday Manara, anakwenda Uholanzi kucheza soka la kulipwa. Baada ya miaka miwili (1978) maisha ya Uholanzi yanamshinda, anaamua kutimkia Marekani kwenye Klabu ya New York Eagles. Mambo bado…

Kina Samatta wapo wengi tu

Nakumbuka kipindi hicho kabla hatujacheza na Nigeria, kocha wa Taifa Stars aliwaita wachezaji wetu kadhaa wa kigeni. Lilikuwa na bado linabaki kuwa wazo zuri sana.  Timu karibu zote ambazo hivi karibuni zimecheza mechi za kutafuta kufuzu zimeundwa na wachezaji wengi…