JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Michezo

Sifa za kijinga

Simba, Yanga lazima zibadilike Na Charles Mateso CECAFA Senior Challenge Cup ya mwaka huu imekuja na maneno mazuri sana kutoka kwa wadau wa soka wa Kenya. Wameamua kutuambia ukweli baada ya miaka kadhaa ya Tanzania kuhangaika na wachezaji kutoka Kenya…

Huku Simba, kule Chalenji, tutampata mkali wetu?

NA CHARLES MATESO Bilionea wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ bado ana kazi kubwa pamoja na ‘sifa’ nyingi za kuwekeza katika uwanja wa Simba Complex, uliopo Bunju, Dar es Salaam. Utazalisha nini? Hilo ndilo swali la msingi la kujiuliza. Una vigezo…

Busara ya Nyerere ifanye kazi Simba

Fedha si msingi wa maendeleo! Haya ni maneno yaliyowahi kutamkwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Yalisemwa miaka mingi kabla dunia haijautambua utandawazi. Tunayaona ndani ya Simba inayotaka kumtimua Patrick Aussems.  Mwalimu Nyerere alimaanisha kwamba fedha ni matokeo…

Tunahitaji nini kutoka kwa Samatta?

Mbwana Samatta ndiye staa wa Tanzania kwenye soka. Ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania. Hili halina ubishi. Kama unataka kupinga hili, unaruhusiwa. Hakuna ubishi kwamba kwenye kikosi cha Taifa Stars, Samatta ndiye mchezaji aliyepiga hatua zaidi. Ndiye mchezaji aliyefanikiwa…

Wachezaji Stars mjiongeze

Leo Taifa Stars itakuwa Stade Mustapha Ben Jannet uliopo mjini Monastir, Tunisia, kuivaa Libya katika mchezo wa kufuzu kuwania kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Huu ni mchezo wa pili, katika mchezo wa awali dhidi ya Equatorial Guinea…

Ya TFF hadi kwa Zahera

Kim Poulsen aliondolewa kazini bila kuwapo sababu zenye kuingia akilini. Alikuwa na  mipango ya kuleta mabadiliko ya uchezaji wa Taifa Stars ndani ya kipindi cha miaka mitano. Waliomuondoa hawakulifahamu suala hilo, ingawa ni jambo muhimu lenye kutakiwa kupewa kipaumbele. Ufundishaji…