JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Uchaguzi Mkuu usituvuruge

Leo tunaumaliza mwaka 2019 na kesho tutaingia mwaka 2020, ambao tunaamini utakuwa ni mwaka utakaotawaliwa na harakati za kisiasa, ikizingatiwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu. Kwanza, tuwatakie Watanzania wote heri ya mwaka 2020, tukiwaombea kwa Mungu wapate…

Hili la ukomo wa urais lisitumike kututoa kwenye reli

  Kwa muda sasa mijadala ya siasa nchini imetawaliwa na suala la ukomo wa mihula ya urais. Katiba inatamka wazi kuwa mtu atashika urais kwa kipindi cha muhula wa miaka mitano na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi cha pili cha…

Serikali isitishe uamuzi wa kujitoa Mahakama ya Afrika

Hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa imeanza mchakato wa kujitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Serikali ilieleza kuwa imeamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona hoja ambazo ilizitoa wakati inajiunga na mahakama hiyo hazijafanyiwa kazi. Tunadhani…

Tulijikomboa ili tuwe huru, tuondokane na dhuluma

Watanzania wameadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika. Hizi ni sherehe kubwa kwa sababu zinaturejesha kwenye kumbukumbu za kazi kubwa iliyotukuka ya ukombozi iliyofanywa na waasisi wa taifa letu. Hatuna budi kuadhimisha siku hii kwa kufanya tathmini ya hali iliyokuwa…

Viongozi acheni kumtegea Rais Magufuli

Kuna kundi kubwa la wananchi ambao wamekuwa wakizunguka katika ziara anazofanya Rais Dk. John Magufuli kwa lengo la kufikisha kero zao kwake.  Watu hao wamefikia hatua hiyo baada ya viongozi na watumishi katika ngazi nyingine kushindwa kuwasaidia kutatua matatizo yao….

Ndugai tafuta busara katika upuuzi wa wanaopinga

Wiki iliyopita Spika wa Bunge, Job Ndugai, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza dhamira yake ya kuliongoza Bunge kutunga kanuni mpya ambazo anaamini zitaleta ulingano kati ya wabunge wa kambi mbalimbali. Spika Ndugai amesema kanuni hizo zitaachana na…