JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Tuwe makini ugawaji mikoa, wilaya

Rais Jakaya Kikwete ametoa baraka za ugawaji Mkoa wa Mbeya ili ipatikane mikoa miwili.

Tayari ameshafanikisha uanzishaji mikoa minne ya Simiyu, Njombe, Katavi na Geita. Pamoja na mikoa hiyo, ameanzisha wilaya nyingi mpya.

vVyombo vya dola visimchekee polisi huyu

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi lilimtia mbaroni mmoja wa askari wake, baada ya kumkuta akiwa na risasi 200 ambazo haijajulikana alikotaka kuzipeleka.

Bravo CHADEMA, CUF mmeonesha ukomavu

Wiki iliyopita, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) vilionesha ukomavu wa kisiasa.

Ardhi itumike kuwawezesha Watanzania

Toleo la leo ni toleo maalum la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Bajeti ya wizara hii imeeleza mipango mingi mizuri yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi nchini na kuwapa Watanzania haki ya kumiliki ardhi.

Wachochezi wa vurugu waadabishwe ipasavyo

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi lilitangaza kumtia mbaroni mtu anayedaiwa kuwa kinara wa kusambaza ujumbe wa kuchochea chuki na uhasama hapa nchini, kupitia simu za kiganjani.

Vurugu za Mtwara ni uhuni na upuuzi

Kwa mara nyingine, wahuni kadhaa katika Mji wa Mtwara jana waliendesha vitendo vya uvunjifu wa amani. Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa, kujeruhiwa na mali za mamilioni ya shilingi zimeteketezwa.