Category: Maoni ya Mhariri
Maskini Bunge letu!
Watanzania tumepata mshituko. Tumeshangazwa na mwenendo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumeshangazwa na jinsi siasa zilivyoanza kugeuzwa uadui. Tumeshangazwa na jinsi wabunge walivyoanza kupoteza heshima na kushindwa kujitambua.
Tuunge mkono mkakati wa TRA
Wiki iliyopita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza mkakati mpya wa ukusanyaji mapato. Mkakati huu mpya ulitangazwa mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini siku ya Alhamisi. Mkutano huo ulimhusisha Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipakodi, Richard Kayombo na Naibu Kamishna (Mapato ya Ndani), Jenerose Bateyunga.
Wabunge msiwaangushe wapigakura wenu
Bunge la Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014 linaanza leo mjini Dodoma, huku Watanzania wakitarajia kuona na kusikia wabunge wao wakipitisha bajeti inayojibu matatizo yanayowakabili.
Waziri Kagasheki asiogope, Serikali isikubali kuchezewa
Machi 26 mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alitangaza uamuzi wa Serikali wa kupunguza eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
Tuoneshe uadilifu Sikukuu ya Pasaka
Machi 31 na Aprili Mosi, mwaka huu ni Sikukuu ya Pasaka, ambapo Wakristo duniani wanakumbuka kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo.
Kamati ya wadau wa habari ituondolee hofu
Wiki iliyopita, wadau wa habari kupitia Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), waliunda kamati ya watu 16 kwa ajili ya kukutana na wakuu wa vyombo vya usalama nchini.