Category: Siasa
KAGAME NI MTIHANI
Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa uangalifu
Kama kuna nchi ambayo imeweza kurithi vilivyo udanganyifu wa kisiasa na unafiki ambavyo himaya kuu ya zamani ya ‘Roma’ ilikuwa navyo, basi ni Taifa kubwa la sasa ‘Marekani’.
Hakika Marekani ndiyo dola kubwa linaloongoza kwa kuwa ‘wakili wa shetani (the devil’s advocate)’.
Katika enzi hizi za Marekani kuwa dola kubwa, yaani kuwa babeli mkuu, damu ya watu wasio na hatia na wasioujua hata huo ubepari wenyewe imemwagika mno na hakuna hata chembe ya soni au hatia ambayo Marekani imejivisha. Hakika imekuwa Roma. Roma ya ustaarabu na sheria vilivyoleta mateso yasiyomithilika.
Kwanini Zanzibar?
Hili ni swali linalogonga vichwa vya wananchi wengi siku hizi. Hivi karibuni kule bungeni Dodoma kulitokea kadhia kubwa iliyosababisha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kususia vikao na kutoka nje ya bunge hili.
Tangu lini wapinzani wanawapenda wananchi?
Vyama vya upinzani vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika Bunge Maalum la Katiba vimesusia vikao vya bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu.
Wapinzani wametoa sababu zao za kuchukua hatua hiyo. Kwa mfano, wamesema Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, wametoa vitisho kwamba kukiwapo Serikali tatu Jeshi litachukua nchi.
Vituko vya DC Geita vyaongezeka – 3
DC adaiwa kumtisha Roboyanke
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyara, Makoye Roboyanke (CCM), ambaye inadaiwa alivuliwa madaraka hayo na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie, amedai kuwa Septemba 10, 2013 mchana akiwa shambani kwake kijijini hapo, alipokea simu ya vitisho kutoka kwa kiongozi huyo wa Serikali.
“Alijitambulisha kwa jina moja la Mangochie na kwamba ndiye Mkuu wa Wilaya ya Geita, akaniuliza jina langu nami nikamjibu… akaniuliza ninachofanya kwa wakati huo na kazi yangu hasa ni nini, nikamwomba arekebishe kauli, na baada ya kurekebisha kauli na kuniuliza maswali ya msingi nilimpa ushirikiano.
KAGAME NI MTIHANI
Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa Uangalifu – 4
Tangu Kagame na RPF waitwae Rwanda ni wazi kuwa nchi hiyo inapokea fadhila za Washington DC kuliko nchi yoyote nyingine katika Maziwa Makuu.
Misaada ambayo inatoka Marekani na Uingereza kuelekezwa Kigali ni mingi na ya aina mbalimbali. Kwa hesabu rahisi misaada hiyo inafafanua ustawi wa uchumi wa Rwanda tunaouona leo.
JWTZ: Tunavifyeka vikundi vya waasi Congo
Baada ya ushindi dhidi ya Waasi wa March 23 (M23), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na Majeshi ya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) limesema hakuna kikwazo chochote cha kuwaondoa waasi wa ADF- NALU na FDRL.