Category: Siasa
Kikwete: Kagame, Museveni, Kenyatta wamenishangaza
Asema wamevuja Mkataba, Itifaki ya Afrika Mashariki
Asisitiza Tanzania inaipenda Jumuiya, haitatoka kamwe
Aonya wasahau ardhi, ajira, kuharakisha shirikisho
Alhamishi wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza mambo manne ya msingi. Amezungumzia mchakato wa Katiba mpya, Operesheni Tokomeza, ushiriki wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na hatima ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kutokana na umuhimu wa hotuba hii, na historia inayoweza kuwa imewekwa na hotuba hii katika siku za usoni, Gazeti JAMHURI limeamua kuchapisha hotuba hii neno kwa neno kama sehemu ya kuweka kumbukumbu na kuwapa fursa Watanzania, ambao hawakupata nafasi ya kuisikiliza hotuba hii, kuisoma na wao pia kuhifadhi kumbukumbu. Endelea…
Tusisukumwe na hoja za kisiasa kujitoa EAC
Katika dunia yetu ya leo ya utandawazi, suala la nchi yoyote duniani kubaki kama kisiwa halipo kabisa. Maendeleo katika teknologia ya mawasiliano yameifanya dunia yetu igeuke kuwa kijiji kimoja.
FASIHI FASAHA
Vyama vya upinzani ni vichanga? -3
FIKRA YA HEKIMA
Bunge likipata Lugola 10 litainyoosha Serikali yetu
Ninatamani kuona siku moja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linafanikiwa kuwa na angalau wabunge 10 aina ya Alphaxard Kangi Ndege Lugola, ambao watatosha kuinyoosha Serikali yetu.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (5)
Huu ni mtiririko wa maandishi yaliyomo kwenye kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1994. Sehemu iliyopita, Mwalimu alisema, “Ni vigumu kuelewa kwa nini watu walio tayari kuwabebesha wananchi mzigo wa SeIikali tatu za kudumu, wanahofu gharama za kura ya maoni ya mara moja! Na kama viongozi wetu ni wapumbavu kiasi cha kwamba hawawezi kutunga swali “Je, unataka Serikali tatu?” Au “Je, unataka Serikali ya Tanganyika?” Kazi hiyo wangeweza kuwaachia wataalamu wenye uwezo zaidi.” Endelea…..
Kwa kutambua kwamba Bunge linafanya uamuzi yake kwa njia ya kura baada ya mijadala ya wazi, Serikali iliona kwamba hoja yoyote kati ya hizi ingewasilishwa bungeni, ingeweza kuligawa Bunge, kukigawa chama chetu na kuwagawa wananchi katika suala zito kama hili la Muundo wa Muungano.
Serikali sikivu inafitiniana, inafitinika
Utawala wa Serikali sikivu chini ya chama tawala unaendelea kuwadhihirishia Watanzania kuwa umefitinika na sasa kila kiongozi anadunda na lake na kauli zake na maagizo yake, bila kujali kuwa uamuzi wao kwa upande mwingine unawaumiza Watanzania ambao kila siku wamekuwa wanasifiwa kuwa Serikali yao sikivu inawasikia.