Na Mwandishi Wetu

Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya CCBRT wameishauri jamii kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara.

Hayo yamebainishwa na Dk. Gaspa Shayo wakati zoezi la kupima afya za wafanyakazi na wateja wa Benki ya NMB likilofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo Septemba 15, 2023.

Dk. Ansila Meneja wa kitengo Macho wa Hospital ya CCBRT akimpima Winnie Lawrence Mtumishi wa Bank ya NMB

Amesema zoezi hilo limeenga kusaidia wananchi kujua afya zao ikiwa ni pamoja na kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara na si kusubiri kuumwa.

“Hili ni zoezi endelevu na kwa kweli litawasaidia watu kujua afya zao kwani ni muhimu sana kujenga utamaduni wa kujua afya yako,” amesema.

Miongoni mwa elimu iliyotolewa kwa watumishi wa benki hiyo pamoja na wateja wao ni pamoja na namba ya kukabialia na mardhi ya Tezi Dume, kufanya uchunguzi wa maradhi ya macho pamoja saratani ya matiti.

Amesema kuwa, uchunguzi huo ni hatua ya awali na kwamba, mtu akibainika kuwa na tatizo, atatakiwa kufika Msasani ilipo hospitali hiyo kwa ajili ya matubabu.

Dk.Gaspa Shayo akimpa elimu ya masuala ya Tezi Dume Mmoja wa watumishi wa NMB

Diana Mtovu, mteja wa benki hiyo aliyepimwa macho, amesema ni jambo jema kwa hospitali hiyo kudhamiria kujenga utamaduni kwa Watanzania kupenda kujua afya zao mapema.

Winnie Laurance ambaye ni mfanyakazi wa benki hiyo, ameeleza kufurahia huduma hiyo na kuiomba CCBRT kuendelea na utaratibu huo.

CCBRT kwa sasa imetanua huduma zake ikiwemo kuwa na huduma ya mama na mtoto na huduma kwa wasojiweza.

By Jamhuri