Wanachama  44 wa CCM wamejitokeza kuwania ubunge jimbo la Korogwe Vijijini.

Wanacham 47 walichukua fomu hizo na 44 kati yao akiwamo mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Thomas Ngonyani wamerudisha fomu hzo.

Jimbo hilo lilikuwa likiongozwa na Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu aliyefariki dunia Julai, mwaka huu.

Katibu wa CCM Wilaya ya Korogwe Vijijini, Suraisa Sangusa amesema tayari makada 44 walikuwa wameshawasilisha na fomu kupokewa rasmi.

Amesema kazi iliyobaki ni kwa kamati ya siasa ya wilaya hiyo kuendesha mchakato wa kuchambua kama waliorejesha wamefuata taratibu zote kabla ya kuyapeleka majina hayo katika ngazi ya mkoa kwa ajili ya hatua ya awali ya mchujo.

Hata hivyo, katibu huyo amesema majina ya waliorejesha fomu na kupokewa

atayataja leo.

“Naomba ifahamike kwamba hawa waliorejesha fomu wataingia katika mchujo wa ngazi ya wilaya, mkoa hadi Taifa ili aweze kupatikana

atakayeaminiwa na chama chetu kupeperusha bendera ya kuliwania jimbo hili dhidi ya vyama vingine,”amesema Suraisa.

Jimbo la Korogwe Vijijini limebaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake Stephen Ngonyani kufariki dunia mwezi uliopita na, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililitangaza rasmi kuwa wazi na kuruhusu vyama vya siasa kuendesha mchakato wa kuwateua wanachama wake kuligombea.

Please follow and like us:
Pin Share