Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kusikitishwa na kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia jana

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu CCM, Dk Emmanuel Nchimbi imeeleza kuwa Mwinyi atakumbukwa kwa mageuzi makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii aliyoyaongoza wakati akiwa Rais wa Tanzania (1990- 1996) , pamoja na jitihada zake za kiutendaji, kiuendeshaji na kimfumo ndani ya chama hicho.

“Sambamba na hayo, daima mchango wake utakumbukwa kwa namna alivyosaidia kujenga umoja wa kitaifa, na kulinda muungano, mojawapo ua tunu zetu za taifa, wakati wa utumishi wake Serikaliā€ imeeleza taarifa hiyo.

Chama cha Mapinduzi kitaendelea kumuenzi mzee Ali Hassan Mwinyi kwa yale yote mema aliyotuusia na kutekeleza

Ali Hassan Mwinyi alifariki dunia Februari 29, 2024 majira ya saa 11:30 jioni katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu

By Jamhuri