Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimewataka viongozi wa dini kuendelea kuikosoa serikali na wasitishwe na mtu yoyote kwani bila wao kusema jamii ya Watanzania itaangamia.

 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,  ametoa kauli hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotokea hapa nchini na hali ngumu ya maisha ya Watanzania ilivyokuwa  mwaka 2017 ambapo aliwanyooshea kidole watendaji wa serikali.

 

Mbowe amezungumzia pia sakata la chama chao kususia chaguzi ndogo za marudio zilizopangwa kufanyika mapema mwakani na akaeleza kwamba Mbunge wa Singida Mashariki,  Tundu Lissu, aliyeko hospitalini  Nairobi, Kenya, ataondoka nchini humo Januari  6 mwaka kesho kwenda kupata matibabu zaidi barani Ulaya.

By Jamhuri