Na Mwandishi, Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila, amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kusajili watoto walio chini ya miaka mitano mara zoezi la kuwasajili watoto hao litalapoanza rasmi jijini mapema mwezi ujao.

Akizungumza kwenye semina ya mafunzo kwa waganga na viongozi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Wakala wa Usajili na Udhamini (RITA) kama sehemu ya maandalizi kabla uzinduzi wa rasmi wa zoezi hilo litakalohitimishwa kitaifa katika Mkoa wa Dar es Salaam. Bw. Chalamila aliiambia semina hiyo kuwa vyeti hivyo vinatolewa bure na kwamba Serikali tayari imebeba gharama zote.

“Nisisikie mwananchi ametozwa pesa ili kupata cheti cha mtoto wake; vyombo vya ulinzi na usalama vipo macho na vinafuatilia kwa karibu sana. Sote tuwe makini na kila mmoja wetu atekeleze wajibu wake”. amesema Bw.Chalamila.

Amewataka wasajili wasaidizi kuhakikisha wanazingatia uadilifu, kujituma na uzalendo na kusema hayo ni mambo ya msingi katika utekelezaji wa mpango huo.

Ametaka viongozi wa dini na wazee maarufu washirikishwe katika utekelezaji wa zoezi hilo..
Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi, alisema kuwa chini ya mpongo huo RITA inategemea watoto 248,298 wasajiliwe mkoani humo, kwani watoto waliosajiliwa ni 624,755 au asilimia 60.3 ya watoto wanaostahili kusajiliwa.

Amesema mpango huo umetekelezwa kwa mafanikio makubwa katika miaka 25 na kwamba Dar es Salaam ndiyo wa mwisho.

“Mikoa 25 ya Tanzania Bara imeshapata huduma isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Hadi sasa zaidi ya watoto 8,886,778 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa ambavyo watavitumia kupata huduma nyingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupata huduma ya matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, elimu sambamba na ajira, alisema Bw. Kanyusi.

“Mikoa 25 ya Tanzania Bara imeshapata huduma isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Hadi sasa zaidi ya watoto 8,886,778 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa ambavyo watavitumia kupata huduma nyingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupata huduma ya matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, elimu sambamba na ajira,” alisema Bw. Kanyusi.

Alisema yamefanyika maboresho na mageuzi makubwa kupitia mpango huo ambapo hivi sasa wamegatua majukumu ya usajili kwenda serikali za mitaa ambapo watoto wanasajiliwa karibu na maeneo yao ya makazi; yaani katika vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto na katika ofisi za watendaji kata,alisema Bw. Kanyusi.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bw Hosea Mitala, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuupa uzito mpango huu, kupitia RITA. Amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchangamkia hiyo fursa hiyo.

Tangu mpango huo uzinduliwe na kutekelezwa katika mikoa 25 wazazi wamewasajili watoto wao kwa bidii na kupata vyeti vya kuzaliwa bure na kuifanya Tanzania isifike kimataifa katika suala hili.