Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameonyesha kutofurahishwa na vinara wa biashara za magendo ambao hupitisha bidhaa mbalimbali katika bandari bubu pasipo kulipa kodi ambapo amesema hali hiyo haivumiliki na hawezi kuifumbia macho hata kidogo.

RC Chalamila amebainisha hayo baada kutembelea na kukagua kipenyo mama cha Magendo eneo la Kunduchi na Bandari ndogo ya Mbweni Wilaya ya Kinondoni.

Chalamila amesema kuendelea kuacha mianya hiyo ya magendo ni kuikosesha kodi Serikali, kuhatarisha Afya za wananchi kutokana na kutumia bidhaa ambazo hazija thibitishwa usalama wake na mamlaka husika ikiwemo TBS vilevile ni hatari kwa usalama wa Taifa ” Ivi karibuni wako watu walipata itilafu ya kiafya kutokana na matumizi ya mafuta ya magendo siwezi vumilia hali hiyo” amesema RC Chalamila.

Vilevile RC Chalamila ametoa siku mbili kwa wachuuzi wa eneo la fukwe ya kunduchi kujitafakari kwa sababu haiwezekani bidhaa hizo zinapita hapo alafu wasijue ambapo amewataka kufanya biashara halali Rais Dkt Samia Suluhu amewekeza nguvu kubwa kutengeneza nchi hivyo wananchi ni lazima waungunge mkono juhudi hizo kwa kukataa magendo kwa masilahi mapana ya Mkoa na Taifa.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amekiri kuwepo kwa Changamoto hiyo na amekuwa akipambana kwa kushirikiana na Mamlaka huisika TRA TBS, na Bandari pamoja na vyombo vya dora lakini namna pekee ni kuendelea na kuongeza nguvu katika ulinzi na kufanya Doria katika mianya hiyo hakuna kinachoshindikana inawezekana kinachotakiwa ni kutimiza wajibu wa kila mmoja wetu.

Please follow and like us:
Pin Share