Michuano ya FA Cup kuelekea hatua ya nusu fainali imepigwa hapo jana kwa michezo miwili ,Wigan Athletic waliondoshwa na Southampton katika michuano hiyo kwa kichapo cha bao 2-0 , huku Chelsea wakichomoza na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Leceister city kwa magoli ya Alvaro Morata na Pedro Eliezer Rodríguez akifunga katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika

Kwa matokeo hayo Southampton na Chelsea zinaungana na Manchester United na Tottenham katika hatua ya nusu fainali,ambapo Chelsea itaivaa Southampton na Manchester United itachuana na Totenham.

Manchester United ilifanikiwa kutinga Hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Brighton kwa magoli ya Romelu Lukaku na Nemanja Matic huku Southampton wakisonga mbele kwa ushindgi wa bao magoli 3-0 dhidi ya Swansea city.

Please follow and like us:
Pin Share