Chongolo ahitimisha ziara yake wilayani Mufindi mkoani Iringa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Daud Yasin (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini (CCM), David Mwakiposa Kihenzile pamoja na Viongozi na wanachama wengine wakitembea kwa miguu kuelekea Nyololo kuhudhuria kikao cha shina namba 27, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 7 mkoani Iringa .

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Halima Dendego (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao cha shina namba 27 lililopo Nyololo wilaya ya Mufindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 7 mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanachama na wanachi wa Nyololo waliohudhuria kikao maalum cha shina namba 27, Nyololo wilaya ya Mufindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 7 mkoani Iringa .Pichani ni moja ya madarasa mapya ya Shule ya Msingi mpya ya Kisalasi inayojengwa na Serikali kupitia mradi wa BOOST iliyopo Kata ya Igowose Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Sehemu ya wakazi wa kata ya Igowose waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya Kisalasi inayojengwa na Serikali kupitia mradi wa BOOST.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema (kulia) wakiteta jambo wakati wa kikao cha nje na wananchi wa Kata ya Ikongosi, Mufindi mkoani Iringa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Katibu wa NEC Oganaizeshi Ndugu Issa Haji Ussi Gavu (kulia) wakati wa kikao cha nje na wakazi wa kata ya Ikongosi, Mufindi mkoani Iringa.

Sehemu ya Wakazi wa Ikongosi  waliojitokeza kwenye kikao cha nje ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Kuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.