Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo ipo Jijini Dar es Salaam wakijiandaa kukabiliana na Yanga SC majira ya 12:15 jioni imemtimua aliyekuwa kocha wake mkuu Yusufu Chippo. 

Taarifa ya klabu iliyotolewa asubuhi hii imedokeza kuwa klabu hiyo itakuwa chini ya kocha msaidizi Sanifu Lazaro mpaka watakapompata kocha mwingine. Sanifu Lazaro ataanza kuisimamia Coastal Union katika mechi ya leo dhidi ya Yanga na mechi nyingine mpaka atakapopatikana kocha mkuu. 

Coastal Union ambao ilikuwa chini ya kocha wa sasa wa Simba SC Juma Mgunda kabla ya kumleta Yusufu Chippo haijaeleza bayana sababu ya kuachana na kocha huyo mkenya.

By Jamhuri