Aliyekuwa daktari wa timu ya Olimpiki Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo.

Katika kesi hiyo mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa kumi.

Alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria.

Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.

‘Nataka ukae jela maisha yako yote’. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia.

Muda mfupi baada ya kutolewa hukumu hiyo, mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nassar kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.

Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.

Bi Simon alikana taarifa kuwa MSU ilifahamu kuhusu tuhuma hizo za unyanyasaji lakini kilishindwa kuchukua hatua.

Katika taarifa yake alisema: “kwa waathiriwa, samahani yangu haiwezi kutosha, kuwa daktari aliyeaminika, aliyefahamika alikuwa ni mtu muovu kwa kweli, aliyewadhulumu kwa kutumia kigezo cha kuwatibu.”

“Ushahidi wa wahanga wa unayanyasaji wa Nassar ni wa kusikitisha, kuvunja moyo na binafsi unaonitia kichefu chefu,” aliongeza.

Takriban wasichana 140 wamewasilisha kesi dhidi ya Nassar, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktarihuyo miaka kadhaa ya nyuma.

Taasisi hiyo ya michezo na chuo hicho zimekana kuwa kulikuwa na chochote cha kufichwa.

Hukumu ya Larry Naser inafuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani mia moja na sitini, wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya olympiki Biles, Aly Raisman, Gabby Douglas na McKayla Maroney

SOURCE: BBC SWAHILI

Please follow and like us:
Pin Share