Watu wengi wamekuwa ni waoga sana wa kupata vipimo vya ugonjwa kutokana na madhara ya kisaikolojia yanayojitokeza baada ya kujua kuhusu ugonjwa, wengi huamua kubaki kwenye hali ya sintofahamu.

Kupitia dalili zifuatazo unaweza kupata mwanga kama umeambukizwa virusi vinvyosababisha ugonjwa wa UKIMWI.

Homa za mara kwa mara, moja ya dalili za mwanzo kabisa zinazoashiria kuwepo wa virusi vya ukimwi ni pamoja na kupanda kwa joto la mwili hadi nyuzijoto 38 hadi 39 ambapo joto hili nalo hupanda mara kwa mara.

Iwapo utapatwa na dalili hii ya homa za mara kwa mara, pia unaweza kupatwa na dalili nyingine zitokanazo na homa hizi kama vile maumivu ya koo, kuvimba kwa baadhi ya tezi za shingo na na mwili kukosa nguvu.

Uchovu, moja ya madhara makubwa ya virusi vya Ukimwi mwilini ni kuathiri mfumo wa kinga mwilini ambapo baada ya mfumo wa kinga mwilini kudhohofishwa na virusi, uchovu uliokithiri ni moja ya matokeo yake. Uchovu uliokithiri unaweza kuwa ishara za mwanzo kabisa za virusi vya Ukimwi. Na uchovu huu huduma hata baada ya virusi hivi kusababisha Ukimwi.

Maumivu ya koo na kichwa yanayodumu, ni kawaida sana kupata maumivu ya kichwa na koo yanayodumu ambayo mara nyingi husababishwa na magonjwa yaa muda mfupi kama vile malaria na magonjwa mengine maumivu ya koo na kichwa.

Lakini pia maumivu ya koo na kichwa yanayodumu kwa muda mrefu yanaweza yakaashiria dalili za maambukizi ya virusi vya ukimwi, hasa yanapodumu kwa muda mrefu.

Afya ya ngozi kubadilika, miezi michache baada ya kupata maamukizi ya virusi vya ukimwi, kuna baadhi ya dalili zinaweza kujitokeza kwenye ngozi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, virusi vya ukimwi vinaenda kupambana na mfumo wa kinga mwilini hivyo mfumo wa kinga ukizidiwa nguvu na virusi hivi, ndipo sasa Ukiwmi unapoanza kuathiri afya ya mwili mzima ikiwemo afya ya ngozi.

Baada ya mfumo wa kinga za mwili kushuka ni rahisi sana kwa ngozi kupata magonjwa ya ngozi ikiwemo chunusi sugu, ngozi kubadilika rangi na kuwa na mabaka mabaka. Japo si wote hupatwa na dalili hii.

Kichefuchefu, kuharisha na kutapika, ni kawaida sana mtu kupatwa na hali hizi mathalani inapotokea mfumo wake wa mmeng’enyo wa chakula umevurugika kutokana na kula au kunywa vitu ambavyo sio salama kwa afya.

Ifahamike kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu wote wanaoishi na virusi vya ukimwi hukumbwa na hali hiyo hasa wakati ambao tayari virusi hivyo vimeshatengeneza ugonjwa wenyewe wa Ukimwi.

Kupoteza uzito (kwa kasi), wakati ambapo virusi vya Ukimwi  vimeshasababisha ugonjwa ni kawaida kwa mgonjwa kupoteza uzito kwa kasi kutokana na kuharisha ambako kunasababisha upungufu wa kiasi kikuwa cha maji mwilini.

Katika kipindi hiki pia ni rahisi sana kwa mtu kupoteza uzito kupita kiasi iwapo atakua anapata mlo hafifu. Kupoteza uzito kupita kiasi na kukonda kwa ujumla sio dalili tu lakini pia ni tatizo la kudumu ambalo mgonjwa anakua nalo kwa muda wote wa ugonjwa huo.

Nimonia na kikohozi kisichoisha, kwa tafsiri ya kawaida ni maambukizi yanayojitokeza kwenye mapafu, mara nyingi inaweza kusababishwa na aina mbalimbali ya vimelea kama vile bakteria, virusi (sio lazima viwe vya ukimwi), au hata fangasi.

Kwa kawaida nimonia ikisha athiri mapafu inasababisha matatizo kadhaa hadi kwenye mfumo mzima wa afya wa upumuaji na hivyo kumsababishia mgonjwa matatizo kama vile, kushindwa kupumua vizuri, kupata homa, kukohoa sana. Kwa ujumla nimonia inasababisha kikozi kisichoisha kwa mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Mabadiliko yanayojitokeza kwenye kucha, dalili nyingine inayojitokeza baada ya kupata maambukizi ya ya virusi vya ukimwi ni mabadiliko yanayojitokeza kwenye kucha.

Kwa tafsiri nyingine ni kwamba mabadiliko hayo ya kucha mara zote yanaongea kitu kuhusu mwenendo afya ya mtu husika na hasa inapofikia kwenye suala la virusi vya ukimwi. Mwathirika huonesha dalili mbali mbali kwenye kucha zake kama vile kucha kuonekana zimekauka, kubadilika rangi, na hata kumeguka.

Hii hutokana na maambukizi ya fangasi yanayoshambulia kucha ambayo huwa yanatokana na kudhohofika kwa mfumo wa kinga mwilini.

By Jamhuri