Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema itahakikisha inashughulikia kwa haraka changamoto zinazopelekea uhaba wa mafuta nchini unahimilika kwa kupitia mfumo mzima wa upangaji wa bei ili kusaidia wananchi kuwapunguzia kiwango cha ukali wa gharama za kupanda bei za bidhaa

Ameyasema halo leo Naibu Waziri Mkuu ambye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika kikao kazi na Watumishi wa EWURA Kanda ya Dar es Salaam alipofanya ziara yake ya kutembelea ofisini hapo ambapo amesema sasa kuna achangamoto ya mafuta nchini na sio Tanzania pekee ni duniani lakini pamoja na changamoto ziko sababu ambazo ni nje ya Tanzania mfano ukosefu wa dola, uzalishaji wa mafuta, gharama kubwa za uletaji wa mafuta.

Lakini ziko sababu lazima ziangaliwe kwa undani ambazo zitasaidia kupunguza mzigo kwa wananchi.

”Tuangalie kuna vitu tunadhani bei zake zimekuwa kubwa zaidi ni kazi ya Ewura kupitia kufanya utafiti kujiridhisha kama hizo chaji ni halisi, tumekubaliana na EWURA na Wakala wa Uagizaji mafuta kwa pamoja na Wizara ya Nishati tutapitia bei upya kwa premium tunazotumia kuagiza mafuta ili tupate bei halisi mafuta ili Watanzania waweze kupata nishati kwa bei nafuu .

“Ila sisemi tunapunguza bei ya mafuta wala ninachosema tunapitia tujiridhishe na bei kama tumeambiwa ni bei kadhaa je ni bei hiyo halisi? ”amesema Dkt.Biteko.

Biteko amesisitiza kuwa timu itafanyia kazi.suala hilo. Suala la upangaji wa bei EWURa kuwa ni jambo linalowapa simanzi wananchi kila wakati bei inapotaka kubadilika, mafuta yanaadimika baadaye mafuta yanaanza kupatikana huo ndio mchezo Watanzania hawawezi kufanyiwa lazima wafanyabiashara wajue pamoja na leseni ya biashara wanayopewa lengo lao ni faida na kukuza mtaji wao,lakini wahudumie Watanzania ili shughuli za uchumi zisitatizike siyo kuwaumiza.

Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara wajue nao wanawajibu wa kuisaidia Serikali kwa leseni walizopewa wafanye kwa uaminifu kwani kiwango cha uagizaji mafuta kimepungua lakini Serikali imechukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa hilo pengo linashughulikiwa mujibu wa sheria.

Sanjari na hayo Dkt Biteko amebaini kuwa ziko taarifa za watu wachache humo ndani ya EWURA wasiowaaminifu wanajihusisha na vitendo vidogo vidogo kwani wakitaka kufanya operasheni wahusika wanakuwa na taarifa siku hiyo hiyo.

” Kwenye tatizo la mafuta mnaenda kukagua mnakuta vituo vimefunga na hawapo ndani ya EWURA kuna watu wanataarifa hizo na wanaenda kuwaambia wanazivujisha na kufanya ukaguzi uwe mgumu.”amesema Naibu Waziri.

Aidha wito umetolewa kwa EWURA kama mdhibiti kuanza kupitia mfumo mzima wa upangaji wa bei kuona kama bei tunazopanga zinakwenda na hali halisi kama kuna shida ya mafuta kutoka kwa wazalishaji wakubwa lakini mahitaji ya mafuta yameongezeka kwa sababu shughuli za kiuchumi zimeongezeka

Watu wanajenga viwanda mahitaji ni makubwa ya mafuta lazima tufikiri jinsi ya kuziba hilo pengo hilo

Sasa Serikali inampango mkakati wa LNG

Magari yanayotumia gesi asilia, kwanini tusiyaongeze. Ewura tuanze na mpango huo ili magari yanatotumia gesi asili yawe mengi zaidi na tupunguze matumizi ya mafuta tuhame kutumia mafuta twende kwenye gesi.

“Hili linawezekana kama sote tutakubaliana tuhame kwenye magari yanayotumia matufa twende kwenye gesi na tuanze na magari ya serikali tubadilishe mfumo wake kwenda LNG tujenge vituo vingi vya LNG.

“Tukipunguza hiyo volume ya magari tutapunguza mafuta yanayotumika mengi yatatumika kwa viwanda” amesisitiza Dkt. Biteko.

By Jamhuri