Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa futari kwa makundi maalum Zanzibar wakiwemo Wazee wa Kituo cha Wazee Sebleni na Watoto kutoka kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini Unguja Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya futari hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee Zanzibar, Hassan Ibrahim Suleiman amemshukuru Makamu wa Rais kwa futari hiyo pamoja na kuwajali wazee na watu wa makundi maalum.

Amesema Futari hiyo kutolewa kwa makundi hayo ni sadaka ambayo Makamu wa Rais amekua akitoa kila mwaka kwa lengo la kusaidia wahitaji.

Viongozi na watumishi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakishiriki futari pamoja na Wazee kutoka katika Kituo cha Wazee Sebleni kilichopo Wilaya ya Mjini na Watoto kutoka kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini kilichopo Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Zanzibar iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kwaajili ya Makundi Maalum tarehe 05 Aprili 2024.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Khamis amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kushirikiana katika mambo yote ya msingi yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, utamaduni na mengineyo ili muungano uweze kudumu daima.

Wazee mbalimbali kutoka katika Kituo cha Wazee Sebleni kilichopo Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar wakishiriki Futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kwaajili ya Makundi Maalum tarehe 05 Aprili 2024.

Amesema serikali zote mbili zitaendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zote zinazokabili Muungano ili kuhakikisha zinaisha kabisa.

Amewasisitiza wananchi kuendeleza umoja na ushirikiano baina ya pande zote mbili ili kuweza kuishi kwa amani na utulivu.

By Jamhuri