Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vina shugulikia migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo inaletwa na baadhi ya viongozi pamoja na matajiri toka nchi jirani .

Ikiwa ni pamoja na kubaini vingozi wanaohusika pamoja na askari polisi wanaoruhusu kupitisha maroli yaliyobeba mifugo na kupewa pesa kwa kila ng’ombe sh.100,000 hadi 120,0000 ambapo kila roli linalopitishwa wanajipatia hadi sh. 5,000,000.

Agizo hilo litolewa leo kwenye uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea ,mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campaign 2023/2025,.

Amesema anataarifa kuwa kutokana na migogoro ya wakulima na wafugaji kuna migogoro ya ardhi mingi inachangiwa na baadhi ya viongozi pamoja na askari polisi ambao wanadaiwa wamekuwa wakila rushwa kwa kupitisha mifugo kinyume na sheria ya nchi, licha ya kuwa serikali imepiga marufuku uingizaji wa mifugo holela mkoani Ruvuma na kutaka viongozi hao na Polisi wachukuliwe hatua.

Amefanua zaidi kuwa, kumekuwepo na vitendo vya ukatili ambavyo vinaongezeka kupitia migogoro ya Ardhi, kwa wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kufanya uharibifu mkubwa hivyo ameitaka vyombo vya usalama kuwachukulia hatua watu wote wanaohusika.

“Ninayo taarifa ya baadhi ya viongozi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na baadhi ya matajiri kuingiza mifugo kinyemela pia wapo baadhi ya Polisi nao wanapitisha maroli yaliyosheheni ng’ombe na wanapata hadi milioni tano , hali ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi “amesem a Dkt.Mpango.

Hata Hivyo Makamu wa Rais Dk.Mpango amesema kuwa kati ya Januari hadi Desemba 2022 vitendo vya ukatili wa kijinsia vimeongezeka sana ambapo matukio zaidi ya 2000 yameripotiwa kai ya hayo ubakaji ni zaidi 6000,ulawiti 5000, mimba za utotoni 1000 na vitaka vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu wote wanaohusika pamoja na kuwafikisha mahakamani .

Aidha, amewaaagiza viongozi kuanzia ngazi ya kata , watendaji na wenye viti wa serikali ya mitaa na vijiji kutoa elimu kwa jamii juu ya ukatili wa kijinsia na pia amewaomba watu wenye uhitaji wa msaada wa kisheria kutumia nafasi hiyo kikamilifu ili waweze kupata haki zao.”Wananchi wapate huduma kwa wakati kupitia kampeni hii ili kuongeza uelewa wa wananchi , juu ya misingi ya haki na upatikanaji wa haki ,kuboresha upatikanaji wa haki hasa kwa watu wasio na uwezo , hasa wananawake ,watu wenye ulemavu , watoto na watu wa makundi mengine,”Alisema Dk.Mipango

Kwa upande wake Waziri wa katiba na Sheria,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt.Damas Ndumbaro ,alisema mkakati huu wa kampeni ya Mama samia unalenga kuongeza uelewa wa msaada wa elimu mkwa wananchi hasa wanyoge na wanaotoka sehemu za Pembezoni na tayari imesaidia mahabusu.

Amesema , kampeni hii inapita kila mkoa , ambapo Ruvuma ni mkoa wa nne tangu kuzinduliwa na imeshapita Dodoma, Manyara, shinyanga na tayari halmashauri 21 zimepitiwa lakini pia inapita kwenye taasisi mbali mbali zinazojishughullisha na elimu ya msaada wa kisheria, na imeshatatua zaidi ya migogoro 2000 ambapo wananchi wameweza kuandika wosia na imetoa haki na usawa kwa wananchi .

Aidha , amewaonya wananchi wenye tabia ya kutoa Lugha za kudhalilisha viogozi ,kwa kuwatukana kwenye mitandao ya kijamii kuacha tabia hizo mara moja na watumie fursa hiyo kutoa maoni yenye staha na sio lugha za matusi

Naye Waziri wanchi ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Suleiman Jaffo amewataka Watanzania kutunza mazingira kwani mwaka jana watakumbuka nchi iliumbwa na shida kubwa ya umeme kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira ambao umesababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Muda si mrefu kuanzia Septemba utasikia Longido wanyama wakifa kwa kukosa maji na uame hivyo watanzania tujitahidi kutunza mazingira ili kuhokoa uoto wa asili.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,.Uratibu na Bunge Jenister Mhagama ,amesmhukuru Rais Samia Suluhu Hassan wa kupeleka maendeeo mkoani hapo ikiwemo miradi ya kimkakati kama reli kutoka Mtwara mpaka Mbambabay kwani itanufaiisha mkoa wa Ruvuma na taifa kwa ujumla ,pia na kujenga miundombinu ya Barabara ya Namtumbo- Mahenge- Morogoro kwa kiwango cha rami.

Nao wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wamempongeza Rais kwa kuona umuhimu wa kuanzisha kampeni ya Msaada wa Kisheria kwani itawasaidia kupata elimu pamoja na kujua haki zao za msingi ikiwemo namna ya kuandika mirathi , wosia , utatuzi wa migogoro ya ardhi paoja na ndoa.

By Jamhuri