Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt .Stargomena Tax amesema suala la amani na utulivu vilivyopo nchini ni moja ya mafanikio ya kazi iliyofanywa na Wizara yake kupitia  sekta ya ulinzi  katika kipindi cha miaka  60 ya Muungano na hivyo kuifanya Nchi kuwa shwari tangu wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi sasa.

Waziri huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi zilizofanywa na wizara yake kupitia sekta ya ulinzi katika ipindi cha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .

 “Katika kulinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uhuru, na usalama wa nchi, Wizara kupitia JWTZ imechangia katika kujenga uchumi imara ambapo wananchi hujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali bila hofu. “alisema na kuongeza kuwa

“Yote hayo yamewezekana kutokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mipango madhubuti katika ulinzi wa nchi, vinavyotoa fursa kwa wananchi kujikita katika ujenzi wa Taifa lao. “

Aidha alisema , Serikali kupitia Wizara imeendelea kutekeleza, na kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu, na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.

Pia alisema mchango mwingine mkubwa wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania katika miaka 60 ya Muungano, ni ulinzi madhubuti wa Mipaka ya nchi , Uhuru, na Katiba.

“Mafanikio mengine ni ushiriki wa Wizara kupitia Taasisi zake, hususan Jeshi la Wananch wa Tanzania (JWTZ)  katika kukabiliana na majanga au maafa mbalimbali pale yanapotokea,

 “Katika kutekeleza jukumu hilo, JWTZ imeendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa misaada ya uokoaji na ile ya kibinadamu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.”

 Kwa mujibu wa Waziri huyo , Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika Miradi ya Kimkakati huku akisema baadhi ya maeneo ambayo JWTZ imeshirikiana na Mamlaka za Kiraia ni pamoja na kushiriki katika kuboresha huduma katika Taasisi za Serikali, kushiriki katika ulinzi wa miradi na maeneo ya kimkakati kwa nchi ikiwemo katika migodi mbalimbali, ulinzi wa miundombinu kama Reli, ikiwa ni pamoja na reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR).

Pia ulinzi wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project – JNHPP), ulinzi katika Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Simu (TTCL), na maeneo ya Viwanja vya Ndege.

 Eneo jingine ni pamoja na utoaji wa huduma za afya na tiba kupitia hospitali za Jeshi za Kanda ambazo ni Lugalo Dar es Salaam, MH Mwanza, Bububu Zanzibar, Mirambo Tabora, MH Arusha, MH Mbeya ambazo hutoa huduma kwa 8 wanajeshi, na pia kwa wananchi waishio maeneo yaliyo jirani na kambi za Jeshi, na katika hospitali nyingi