Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akishuhudia utiaji saini wa makubalino ya awali ya ujenzi wa kiwanda cha saruji kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka katika Wilaya ya Kongwa. Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki kati ya kampuni ya 
Alotab & Block BB na Libyan Petrolium ya Libya. Hafla hiyo imefanyika mbele ya wajumbe wa Baraza la Ushauri Mkoa wa Dodoma jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libya, Dmjed Rajab (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha saruji wilayani Kongwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule  akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubalino ya awali ya ujenzi wa kiwanda cha saruji kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka katika Wilaya ya Kongwa. Uwekezaji wa Kiwanda hicho utagharimu dola za kimarekani milioni mia mbili. Kiwanda hicho kitasaidia kuleta ajira na kuinua pato la mkoa na Taifa kwa ujumla ambapo makubaliano ya walimu ujenzi wa kiwanda cha saruji uiwekezaji wake ni wa thamani ya dola milioni 200.

By Jamhuri