Real Madrid jana usiku mambo yao yamezidi kuwaendea kombo baada ya kuchezea kichapo cha bao 10 kutoka kwa Espanyol, kipigo hicho kinaifanya Real Madrid kupoeza jumla ya michezo mitano ya LaLiga msimu huu, goli pekee la Espanyol limefungwa na Gerard Moreno katika dakika ya tatu za nyongeza kabla ya game kumalizika.

Ushindi huo sasa unaifanya Espanyol kufanikiwa kuviadhibu vilabu vyote vikubwa Hispania katika LaLiga vilivyocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid wote msimu huu wamepoteza kwa kufungwa goli 1-0, Espanyol wanafanikiwa kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Real Madrid baada ya miaka 11.

Katika michezo 23 ya LaLiga ambayo Espanyol alicheza na Real Madrid toka 2007, amefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee kwa goli 2-1, Espanyol wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani September October 20 2007, sare game tatu pekee na kuruhusu kufungwa game zote 19 zilizosalia, hivyo leo wanaweza kufanya sherehe kwa kuvunja rekodi hiyo.