Kaimu Meneja Mkuu Kampuni ya ETDCO CPA Sadock Mugendi amesema wanaendelea kujenga miundo mbinu ya umeme nchini ikiwemo njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi ambao ni mradi wa kusafirisha umeme na tayari mradi umefkia asilimia 67.

Mugendi amesema ETDCO ni kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania na ni suluhisho la miundombinu ya umeme kwani ipo kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundo mbinu ya kusafirisha na kusambaza umeme.

Kaimu Meneja Mkuu CPA Sadock amesema Mradi wa kutoka Tabora kwenda Katavi wenye irefu wa kilometa 383 wa msongo wa 132kV ambao unatarajiwa kumalizika mwaka huu na kupelekea Mkoa wa Katavi kupata umeme wa uhakika pia Kuipunguzia Gharama TANESCO za Kununua mafuta ya Dizeli kwajili ya Jenereta ili kuzalisha umeme kwenye Mkoa Wa Katavi.

CPA Sadock ameipongeza Serikali kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya nishati ili kuhudumia wananchi wake vizuri, amesema Hayo wakati Akitembelea mradi wa kimkakati wa Tabora kwenda Katavi wenye msongo wa 132kV.