FAWOPA Yapiga Msasa Wadau wa Elimu-Mtwara

Pichani ni mratibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la faidika wote pamoja FAWOPA iliyopo Mkoani Mtwara Baltazar Komba akizungumza na wadau mbali mbali wa elimu juu ya Uboreshwaji wa Elimu mkoani Humo.
Mshauri wa Mambo ya Kisheria FAWOPA Marythereza Namangi akitoa mafunzo kwa Wadau Mbalimbali wa Elimu Juu ya uandaaji wa Bajeti katika mashule kama Moja ya Dhana ya Uwazi na Uwajibikaji.
Shirika lisilokuwa la kiserikali la faidika wote pamoja FAWOPA limetoa Elim kwa Wadau Mbalimbali wa sekta hiyo Juu ya uandaaji wa Bajeti na kuweza kuwasilisha kwa kamati za Shule ili kuweza kuzifanyia kazi Kwa lengo La kuondokana na migongano inayojitokeza baina ya Wazazi na Walim.
Mratibu wa shirika hilo Baltazar Komba amesema Bado viwango vya Bajeti mashuleni haijaainisha matokeo yake Shule Nyingi wamekuwa wakitegemea wazazi kwa ajili ya michango kabla ya Mh. Rais John Pombe Magufuli kukataza Michango yoyote Mashuleni.
Aidha katika Ufatiliaji uliofanywa na Kamati ya FAWOPA ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani imebaini kuwa Halmashauri haina Bajeti maalum ya Elim zaidi ya Bajeti kutoka Serikali Kuu.
Lengo la mkutano huo ni kuhakikisha manispaa hiyo inapiga hatua katika swala la elimu kutokana mkoa was Mtwara kuwa nyuma katika Ufaulu ukilinganisha na mikoa mwingine.