Na Mwandishi Wetu

HALOTEL ikiwa kampuni inayosifika nchini kupitia huduma zao za kifedha za HaloPesa, inaendelea kuwahamasisha wateja wao kwa kuleta huduma za ubora na zenye ubunifu, na wakizindua kampeni ya Shida Tena na Halopesa leo.

Wakiwa kampuni inayokua kwa kasi sana HaloPesa, imeendelea kutoa huduma za kifedha kwa wateja wao na wanaendelea kuja na huduma mbalimbali zenye gharama nafuu ambazo zinafika kote mjini na kijijini Tanzania.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za Halotel Tanzania, Naibu Mkurugenzi Mkuu Magesa Wandwi alisema “Huwa tunafuraha kubwa kutoa huduma hizi za kifedha, na kuwawezesha wateja hususani wateja wa HaloPesa kufanya miamala tofautitofauti kama kutuma pesa kwenda HaloPesa, kutuma pesa kwenda mitandao mengine, kutuma pesa kwenda benki, kulipia billi, Lipa hapa nakadhilika. Zaidi ya wateja 2.5m ambao ni wateja hai wanaendela kufurahia huduma zenye ubora na kwa gharama nafuu muda wowote.

Naibu Mkurugenzi Mkuu Halopesa, Bw: Magesa Wandwi: akiongea na Waandishi wa Habari leo katika Uzinduzi wa Kampeni Mpya ya Halopesa iendayo kwa jina la Shinda Tena na HaloPesa  ambayo itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu (3) na jumla ya wateja 135 watakuwa washindi. Jumla ya  wateja 120 watashinda pesa Taslimu na  jumla ya wateja 12 watashinda Luninga Janja na wateja watatu 3 watashinda Bajaji mpya. Tutakua na washindi wa kila siku ambao watashinda pesa Taslimu na washindi wa kila wiki wa Luninga janja na washindi wa kila mwezi ambao watashinda Bajaj.

Kampeni ya Shinda Tena na HaloPesa ni kwa ajaili ya kuhamasiha na kuwapa motisha wateja wa HaloPesa ili waweze kuendelea kutumia huduma zetu lakini pia kuwapa chachu wateja ambao hawatumii huduma hizi za kifedha za kidijitali waweze kuingia kwenye ulimwengu huu. Ni ndoto yetu kuona watanzania wote wanatumia huduma za kifedha kiganjani mwao. Aliongezea Magesa

Kampeni ya Shinda na HaloPesa ni kwa ajili ya wateja wa HaloPesa ambayo itakuwepo kwa miezi mitatu (3) na jumla ya wateja 135 watakuwa washindi. Ambao wateja 120 watashinda pesa Taslimu na wateja 12 watashinda Luninga Janja na wateja watatu 3 watashinda Bajaj mpya. Tutakua na washindi wa kila siku ambao watashinda pesa Taslimu na washindi wa kila wiki wa Luninga janja na washindi wa kila mwezi ambao watashinda Bajaj.

Naibu Mkurugenzi Mkuu Halopesa, Bw: Magesa Wandwi: akiwa na Afisa Masoko  Halopesa Roxana Kadio wakikata utepe mbele ya wandishi wa habari leo kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa Kampeni Mpya ya Halopesa iendayo kwa jina la Shinda Tena na HaloPesa  ambayo itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu (3) na jumla ya wateja 135 watakuwa washindi. Jumla ya  wateja 120 watashinda pesa Taslimu na  jumla ya wateja 12 watashinda Luninga Janja na wateja watatu 3 watashinda Bajaji mpya. Tutakua na washindi wa kila siku ambao watashinda pesa Taslimu na washindi wa kila wiki wa Luninga janja na washindi wa kila mwezi ambao watashinda Bajaj. 

Kila mteja wa HaloPesa anaalikwa kushiriki kwenye promosheni hii kwa kufanya miamala ifwatayo; Kutuma hela HaloPesa kwenda HaloPesa, Kutuma hela mitandao mengine, kutuma hela benki, Malipo ya serikali, Lipa billi, Lipa Hapa, kutoa kupitia wakala, kutoa hela kutoka ATM pamoja na miamala ya HaloYako. Mteja ataongeza nafasi yake ya kushinda zawadi, hivyo tunawahamashisha wateja wetu kufanya miamala mingi ili waweze kupata nafasi kubwa ya kushinda zawadi hizi kabambe. Alisema Magesa.

HaloPesa inafurahia kuzindua promosheni hii leo na itaendelea kufikiria njia nyingine Zaidi za kufanya ulimwengu wa huduma za kifedha kupitia simu kuwa bora Zaidi kwa ajili ya wateja wetu.