Wizara ya afya ya Ukanda wa Gaza inayoongozwa na Hamas imesema leo Jumamosi kuwa takriban watu 32,142 wameuwawa huku wengine 74,412 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita kati ya vikosi vya Israel na kundi la Hamas.

Uharibifu unaotokana na mapigano yanayoendelea Ukanda wa Gaza

Taarifa hiyo imeongeza kwamba idadi hiyo inajumuisha pia vifo 72 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Katika hatua nyingine jeshi la Israel limesema kuwa limewauwa watu 170 wenye silaha katika oparesheni ilioifanya katika hospitali ya Al Shifa, na kuwahoji washukiwa wengine zaidi ya 800, huku wakigundua silaha nyingi pamoja na miundombinu mingine ya kigaidi.

Al Shifa, hospitali kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza kabla ya vita, sasa ni mojawapo ya vituo vichache vya huduma za afya vinavyofanya kazi kaskazini mwa eneo hilo, na pia imekuwa ikihifadhi raia waliokimbia makazi yao.

By Jamhuri