Happy Nation lagongana uso kwa uso na roli

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Morogoro

Watu wanne wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Mkambalani wilayani Morogoro ikihusisha basi la abiria kampuni ya Happy Nation lenye namba za usajili T 702 DGF lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Jijini Mwanza kugongana uso kwa uso na roli la mizigo lenye namba za usajili T179 DCR lililokuwa likitokea Zambia kuelekea Dar es Salaam.

Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Morogoro ACP Ralph Meela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo chanzo cha ajali kinadaiwa na uzembe wa dereva wa basi hilo Hassan Abdalah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lingine (overtake) bila kuchukua tahadari na kusababisha ajali hiyo.

Mashuhuda wa ajili hiyo wmeasema dereva alikua anajaribu kuyapita magari mengine nane ndipo alipoashindwa na kijikuta anaingia upande ambao sio wake.