Na Mwandishi wetu, JAMHURI MEDIA

Ibada ya kumbukumbu ya Mwanamziki Constantinos Tsobanoglou maarufu “Costa Titch” aliyefariki jukwaani, iliyotarajiwa kufanyika Alhamisi Machi 16, 2023 imeahirishwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya mwanamuziki huyo imeelezwa kuwa, kuchelewa huko kumetokana na baadhi ya mashabiki waliopewa jina la “Titch Gang”, ndani  na nje ya Afrika Kusini kushindwa kufika kwa wakati kutokana na taarifa  iliyotumwa mda mfupi .

“Kama tunavyojua, Costa alihusu ushirikishwaji na umoja, angependa kuwa na kila mtu ambaye alimpenda na anayemuunga mkono kuwa hapo.

“Asante kwa kuelewa na upendo wako na msaada unaoendelea ambao umeonyesha familia, marafiki na timu.”

Familia imesema itatoa tena  tarehe mpya na mahali itakapofanyika ibaada hiyo, ambayo itarushwa mubashara kupitia  Chaneli  yake ya YouTube.

Mpaka sasa familia hiyo haijadokeza ni lini na wapi mazishi ya mwanamziki huyo  yatakapofanyika japokuwa inaelezwa kuwa watatoa taarifa hiyo hivi karibuni

Wasanii, watu maarufu Pamoja na kundi maarufu la ‘Titch Gang’ wanaendelea kumuenzi msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii

Costa Titch Rapa na dancer mwenye umri wa miaka 28 kutoka Mpumalanga alianguka na kufariki dunia alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la Ultra Music katika ukumbi wa Expo Centre mjini Johannesburg mnamo Machi 11, 2023.