Licha ya Ihefu kuwa bora kwenye mchezo wa leo mbele ya Simba kwenye upande wa umiliki wamekwama kuondoka na pointi tatu.

Dakika 90 zimekamilika ubao wa Uwanja wa Highland Estate unasoma Ihefu 0-2 Simba.

Mabao yote mawili yamefungwa na Jean Baleke kipindi cha pili katika dakika za lala salama ilikuwa dakika ya 83 na 86.

Simba inafikisha pointi 60 ikiachwa pointi 5 na Yanga iliyo nafasi ya kwanza lakini Yanga ina mchezo mmoja mkononi ikiwa imecheza mechi 24 Simba 25.

By Jamhuri